Lyrics to Leah
Leah Video:
Leah - Dully Sykes / Tanzania Nilimkuta Leah amejilaza Chini kwenye kituo cha wamataa Huku ngozi yake maji ya kunde Imegeuka ya majani isiyopendeza Unafanya nini nikamuliza ? Akanijibu anaumwa na pia ana njaa Msichana wa miaka wa kumi na tisa Kumbe alikuwa amesha hadhirika Nikampeleka duka la madawa Hili kidonge kidogo imweke sawa Kwani alikuwa na fungus mwili mzima Ikambidi anihadhithia stori nzima Akaanza kuniadhithia kwa huruma Kwamba siku mmoja alikuwa anatoka shuleni Siku hiyo njaa ilimtawala Akotokea dereva wa daladala Akamwambia Leah Lifti panda mbele Japo mwanafunzi akae kiti cha mbele Tena bila malipo ni burebure Akaanza kumtongoza polepole Sababu Leah njaa ilimtawala Akaambiwa atanunuliwa Chipsi, Soda Ilipofika jioni akanunuliwa Wakapanga wakutane tena Palepale Ilipofika Wakakutane palepale Akapanda daladala hadi usiku Wakaenda kufanya yao mavitu Wakaenda kufanya yao mavitu (Refr) Leah Umekwenda Hayo yote Mola amepanga 3x Akamrubuni nakumfanya mapenzi Akawa akitoka schule yeye kwa mchizi Kwa bahati Leah schule alimaaliza Baada ya tu kumaliza akatoroshwa Akaishi na yeye Kama mke na mume Nyumbani alikuwa na magokumu yote Kuosha viombo kupika na khadhalika Ikawa akikosa kidogo anapigwa Baada hema na mume akawa na kisirani Alivumilia mpaka mwisho akashika mimba Alikaa nayo mpaka miezi tisa Aliyifungulia huko muhindili Mtoto akafa baada ya miezi miwili Alikufa kwa ugonjwa wa Nimonia Baadaye pia aliuguwa Alikuwa na tatizo la kifua Tubercolosis oh liliyomsumbuwa Muda wa wiki mbili alisumbuliwa Ilipofika Tarehe sita mwezi wa kumi Nakumbuka siku hiyo ilikuwa jumapili Ndiyo siku hiyo Leah alifariki Ilipofika jumanne tarehe nane Ikabidii watu wote tuungane Tukamzika tabata makaburi Hapo ndipo yalikuwa makaburi Mungu mlaze mahali pema peponi x 2 Leah




Songwriters:
Publisher:
Powered by LyricFind